Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwakyembe azisifu Mwananchi, KPMG kuhamasisha uchumi wa viwanda

24069 Mwakyembe+pic TanzaniaWeb

Sat, 27 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Dk Harrison Mwakyembe amesema Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) na KPM ni wadau wakubwa wa Serikali katika ujenzi wa uchumi wa viwanda.

Waziri Mwanyembe ni mgeni rasmi katika fainali za mashindano ya Top 100 zinazoendelea hivi sasa katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini hapa.

Mwanyembe amesema ameagizwa na Waziri Mkuu kumuwakilisha katika tukio hilo kutokana na umuhimu wa kampuni za kati nchini.

"Kampuni za kati zina mchango mkubwa katika uchumi wa nchi, kulipa kodi, kutoa ajira kwa Watanzania na kukuza ujuzi…ndio maana mlipomualika Waziri Mkuu alinituma nimuwakilishe kwa kuwa yeye amebanwa na majukumu ya kiserikali," amesema.

Amesema KPMG na MCL ni wadau muhimu katika kufanikisha mpango wetu wa uchumi wa viwanda kutokana na hamasa zinazofanya kuzikuza kampuni za kati.

Katika hatua za awali, kampuni za Sayona Drinks Limited, AMC Tanzania Limited na CSI Electrical Limited zimehitimu kutoka Top 100 na kuingia Klabu 101.

Mashindano ya Top 100 huhusisha kampuni ambazo mapato yake kwa mwaka ni kati ya Sh1 bilioni mpaka Sh20 bilioni na zile ambazo huzidi hapo huingia Klabu 101.

 

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz