Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mvutano EWURA na wasambazaji gesi kuhusu bei mpya sokoni leo

Gesi Bei ya gesi kupanda

Thu, 12 Aug 2021 Chanzo: Mwananchi

Wakati Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) ikisema bei ya gesi za majumbani haitapanda, mawakala wa usambazaji na uagizaji wa gesi wamesema kuanzia leo Alhamisi Agosti 12, 2021 gesi hiyo itapanda bei.

Agosti Mosi, 2021 zilisambaa taarifa za kupanda kwa bei ya gesi ambapo mtungi wa gesi wa kilo13 ulipanda kutoka Sh50,000 hadi Sh53,000 na kilo sita ukiuzwa Sh23,000 kutoka Sh21,000 hali ambayo ilileta taharuki kwa wananchi. Kufuatia kupanda kwa bei hiyo mpya ya gesi Ewura walisitisha bei hiyo Agosti 3, 2021 baada ya wananchi na watumiaji wa gesi hiyo kulalamika.

Akizungumza leo meneja wa Ewura Kanda ya Kaskazini, Lorivii Long'idu amesema gesi haitapanda bei na badala yake wanapitia mawasilisho yaliyowasilishwa na mawakala hao wakitaka bei mpya ya gesi.

"Tulitumia kampuni ambayo ni wasambazaji na wauzaji wa gesi za majumbani kusitisha bei mpya ambazo walikuwa wametangaza, hizi bei walipaswa watushirikishe kabla ya kutangaza mpya.”

"Tunataka watuambie kwa nini bei ya gesi iongezeke na nini kimetokea hivyo tunaendelea na hili zoezi la kupitia mawasilisho hayo wakati tukisubiri kupitia hayo mawasilisho yao bei zitaendelea kubaki zilezile za awali mpaka hapo tutakapotoa maagizo mengine baada ya kujiridhisha na kupitia mawasilisho yao,"amesema.

Chanzo: Mwananchi