Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mvua zasimamisha uzalishaji wa sukari kiwanda cha SBL

Sukarisssssssssss Mvua zasimamisha uzalishaji wa sukari kiwanda cha SBL

Sat, 16 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini Tanzania, zimesababisha kiwanda cha Bagamoyo Sugar Ltd (BSL) kusitisha uzalishaji wa sukari kwa muda.

Kiwanda hicho kinachomilikiwa na Kampuni za Bakhresa, kimesitisha uzalishaji kwa siku 47 sasa, kutokana na mashamba ya miwa kujaa maji, hivyo kushindwa kuvuna miwa.

Hayo yamesema leo Ijumaa Desemba 15, 2023 na Waziri wa Kilimo, Hussei Bashe alipotembelea kiwanda hicho pamoja na mashamba ya miwa kwa lengo la kujionea uzalishaji wa sukari na changamoto zilizopo.

“Kiwanda hiki kilianza uzalishaji mwaka jana na kilizalisha tani 18,700 na mwaka huu walitarajia kuzalisha tani 30,000, lakini kutokana na changamoto ya mvua wamesema asilimia 40 ya shamba la miwa limeathirika na mafuriko," amesema Bashe;

Amesema kama wizara wamejipanga kutatua changamoto za ukosefu wa sukari nchini kwa kuboresha viwanda vilivyopo, ili kukabiliana na uhaba wa sukari nchini.

Matarajio ya Serikali kwa mwaka 2023/2024 ni kuzalisha tani 445,000 za sukari nchini, lakini mpaka sasa imezalisha tani 295,000.

Kuhusu ombi la BSL kwa Serikali kutaka waongezewe eneo kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa kilimo cha miwa, Waziri Bashe wamewataka kuandika barua ya maombi, ili wakae na halmashauri husika  na kujadili.

Kuhusu ombi la kuchimbiwa bwawa litakalotumika kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji, Waziri Bashe amesema tayari imeshatenga eneo kwa ajili ya kuchimba bwawa na wameshakutana na Tume ya Umwagiliaji, Bonde la Mto Wami, Bodi ya Sukari pamoja na kiwanda hicho kwa ajili ya kufanikisha jambo hilo.

"Sisi kama wizara tayari tushatenga eneo kwa ajili ya ujenzi wa bwawa la maji na sasa usanifu wa michoro unaendelea, litakapokamilika wakulima wadogowadogo wanaozunguka kiwanda hiki cha BSL, wataweza kulima miwa na kwenda kuuza kiwandani hapo," amesema.

Katika hatua nyingi, Bashe ameiomba Kampuni za Bakhresa kuangalia namna ya kuwekeza katika kilimo cha ngano na mafuta ya kupikia, kwani kuwepo kwa wawekezaji wakubwa kama yeye kutasaidia Serikali kuachana na uingizaji wa mafuta ya kula kutoka nje ya nchini.

"Nimeomba tukae na  Bakhresa ambaye ni muingizaji mkubwa wa ngano nchini, tujadiliane tuone tunafanyaje, kwa sababu tayari Serikali tumeshatengeza sheria ndogo ya mwaka huu ya kudhibiti uingizwaji wa ngano na mafuta ya kula kutoka nje ya nchini," amesema na kuongeza;

"Lakini hatuwezi tu kudhibiti uingizwaji wa mafuta na ngano bila kuweka mipango, hivyo kama Serikali tumeshaanza kuzalisha mbegu za kutosha za mazao hayo ili kukabiliana na hali hiyo."

Amesema tayari kuna maeneo kwa ajili ya kilimo hicho, mwekezaji huyo atakwenda kuangalia katika Mkoa wa Katavi na Tabora.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni za Bakhresa Group, Hussein Sifiani amesema eneo hilo la kiwanda lina ukubwa wa hekta 10,000.

Hata hivyo, upandaji wa miwa katika awamu ya kwanza umehusisha hekta 2,000 na ujenzi wa kiwanda cha sukari kitakachosindika tani 1,500 za miwa kwa siku.

"Ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha sukari chenye uwezo wa kusindika tani 1,500 za miwa kwa siku, ulikamilika mwaka 2022 na kwa kipindi hicho tulizalisha tani 18,700 za sukari," amesema.

Akizungumzia changamoto, Sufiani amesema wanakabiliwa na uhaba wa maji kwa ajili ya umwagiliaji hasa wakati wa kiangazi, hivyo kuiomba Serikali iwajenge bwawa la maji kutoka mto Wami.

Mpaka sasa kiwanda cha kuzalisha sukari cha Mtibwa, Kilombelo, Kagera na TPC Moshi vimesimamisha kwa muda uzalishaji wa sukari kutokana na mashamba kujaa maji ya mvua.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live