Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mvua yakwamisha treni Kigoma - Dar, abiria 648 wasota Dodoma

90439 Abiria+pic Mvua yakwamisha treni Kigoma - Dar, abiria 648 wasota Dodoma

Tue, 31 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini nchini Tanzania, Patrobas Katambi ameagiza abiria waliokuwa wakisafiri kwa treni kutoka mkoani Kigoma kwenda jijini Dar es Salaam kurudishiwa nauli zao.

Uamuzi huo wa Katambi unakuja kufuatia abiria hao kukwama Dodoma kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha kuifunika reli hiyo.

Katambi ametoa agizo hilo leo Jumanne Desemba 31, 2019, kwa Stesheni Meneja wa Dodoma, Rose Ngauga kuwa ahakikishe abiria hao wanarudishiwa nauli ili kuwahi shughuli zao walikokuwa wanakwenda.

“Ninyi mpo hapa  Dodoma lakini kuna treni nyingine imesimamishwa Kilosa mkoani Morogoro na maeneo mengine maji yamefunika reli haionekani, kwa hiyo si rahisi kwa viongozi wenye akili timamu kama hawa wa TRC kuwaruhusu abiria wao wapite pale kwa kubahatisha.”

“Kutokana na hayo uamuzi ni kuwa, kama suala hili halitafanyiwa marekebisho haraka iwezekanavyo ndani ya saa mbili ni lazima wapewe chakula, kurudishiwa nauli ili waweze kuwahi na wakati huo huo Serikali inafanya hatua ya kuwaita wamiliki wa mabasi haraka, ili yale yaliyopo yatumike kuwafikisha salama na yatakaguliwa,” alisema Katambi.

Mmoja wa abiria hao, Abdallah Sufiani ameishukuru Serikali kwa kuingilia suala lao mapema na kulitatua kwa Mkuu wa Wilaya kuagiza warudishiwe nauli zao pamoja na kuagiza wapatiwe chakula.

Chanzo: mwananchi.co.tz