Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mvua kupunguza mavuno ya mahindi kwa 30%

75a62ec6d844696dbe2605e632573e89 Mvua kupunguza mavuno ya mahindi kwa 30%

Tue, 28 Sep 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MAVUNO ya mahindi katika mwaka huu yanatarajiwa kupungua kwa asilimia 30.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Hamadi Boga, alisema uzalishaji katika misimu miwili ya mvua ndefu na mvua fupi, imeshuka hivyo na kusababisha upungufu wa chakula.

Boga alisema wastani wa mvua za muda mrefu za mavuno ni takribani mifuko milioni 36 ya mahindi.

"Lakini mwaka huu tunakadiria kupata takribani mifuko milioni 28 ya mahindi kutokana na mavuno ya mvua za muda mrefu kuwa pungufu, maeneo mengi yalipata mvua kwa asilimia 30,” alisema.

Idara ya Hali ya Hewa imeeleza kuwa, katika mwezi Oktoba-Novemba-Desemba inakadiriwa kuwa mvua zitakuwa pungufu katika maeneo mengi ya nchi.

Boga alisema kuwa kwa makadirio hayo kutakuwa na uzalishaji mdogo na kuwa, mavuno yanayotarajiwa katika mvua za muda mfupi kwa kawaida ni mifuko milioni saba, lakini mwaka huu wanakadiria karibu mifuko milioni 3.5.

"Lazima tuangalie hili katika mipango yetu ya mwaka ujao, kufikia Desemba na bado tutakuwa na chakula na bei bado zitakuwa sawa,” alisema.

Alieleza kuwa wanatarajia kuagiza mahindi kutoka Uganda na Tanzania kati ya Januari na Februari, lakini wataendelea kufuatilia uzalishaji wa ndani na katika nchi za Uganda na Tanzania,” alisema Boga.

Kulingana na takwimu za hali ya chakula iliyokadiriwa kufikia mwishoni mwa Oktoba, kutakuwa na ziada ya mifuko milioni 18.2 ya mahindi, mifuko milioni 6.9 ya maharage, mifuko milioni 3.1 ya ngano na mifuko 200,000 ya mchele.

Chanzo: www.habarileo.co.tz