Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muwekezaji atoa neno kwa Rais Samia

Msina V Muwekezaji akiwa na sehemu ya ujumbe toka BoT

Thu, 17 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muwekezaji wa kiwanda cha kukata, kung’arisha na kuuza mawe ya asili aina ya Marbo na Granites jijini Mbeya ameipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wake Rais Samia Suluhu Hassan kwa mipango, mikakati na jitihada za kizalendo kwa kuinua uchumi wa nchi hii ikiwemo uchumi wa viwanda.

Akizungumza wakati wa ziara ya waandishi wa habari waliotembelea kiwanda hicho kinachomilikiwa na kampuni ya Marmo E Granito Mines (T) Limited ikiwa ni sehemu ya mafunzo yaliyoandaliwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ili kuwajengea uwezo wa kuandika kwa usahihi masuala ya Uchumi, Biashara na Fedha, Afisa Utawala na Rasilimali Watu wa kiwanda hicho, Bw. Brinton Kulinga alisema mipango ya serikali imesaidia kukifanya kiwanda hicho kuendelea kupiga hatua tangu kilipoanzishwa hadi hivi sasa.

Alisema kiwanda hicho kilichoko eneo la viwanda Iyunga jijini Mbeya awali kilikuwa kidogo na kilitumia teknolojia ya kizamani na yenye uwezo mdogo wa kuzalisha mali na hivyo kazi kubwa ilikuwa ni kusafirisha mali ghafi nje ya nchi

Alisema baada ya kufungwa kwa mitambo mipya yenye kutumia teknolojia ya kisasa kwa sasa kichakata Marbo na kutokana na mipango mizuri ya serikali, kampuni inao mpango mwingine zaidi wa kuendelea kupanua kiwanda hicho cha kipekee hapa nchini na Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Alisema, kuwepo kwa mradi huu sio tu kunautangaza mkoa wa Mbeya katika ramani ya Dunia bali pia taifa kwa ujumla ukizingatia bidhaa zinaendelea kuenea katika soko la ndani na la kimataifa na hivyo kutoa fursa ya kuongeza ari ya uzalishaji ili kukidhi mahitaji ya soko.

Akieleza ubora wa bidhaa zinazozalishwa kiwandani hapo baada ya kazi ya kuchakata mawe hayo makubwa aina ya Marbo na Granites, Mkurugenzi Mtendaji Bw. Salim Jesa alisema, wanatengeneza tiles, meza, ngazi, na mapambo mbalimbali na kwamba kwakuwa bidhaa hizo zinatokana na mawe ya asili hakuna sababu ya kutumia kemikali (sabuni) iku kusafisha bali mtumiaji anahitaji maji tu ili kusafisha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live