Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mususa azitaka kampuni nyingi zaidi kushiriki Top 100

24066 MUSUSAAAA TanzaniaWeb

Sat, 27 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Bodi ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Leonard Mususa amezitaka kampuni nyingi zaidi kujitokeza na kushiriki mashindano ya kampuni 100 bora za kati (Top 100).

Amesema hayo katika hafla ya fainali inayoendelea hivi sasa, leo Oktoba 25, katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini hapa ikiwa ni mwaka wa nane tangu yalipoanzishwa mwaka 2011.

Mususa amesema mashindano hayo yanatoa fursa kwa wafanyabiashara wa kati kukutana na kubadilishana mawazo ya namna ya kukuza biashara zao.

"Washiriki wanapata nafasi ya kujifunza uendeshaji bora wa biashara, kujitangaza na kupata masoko mapya. Hili ni jukwaa kwa wafanyabiashara wa kati kukua zaidi," amesma Mususa.

Chanzo: mwananchi.co.tz