Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtwara waanza kutumia gesi ya kupikia majumbani

Wed, 18 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mtwara. Baadhi ya wakazi wa mkoa wa Mtwara nchini Tanzania kwa sasa wataondokana na matumizi ya kuni na mkaa baada ya kuunganishwa huduma ya gesi majumbani kwa ajili kupikia lakini pia kuhifadhi mazingira.

Kwa kuanza wateja 125 kati ya 310 wameunganishwa na huduma hiyo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo leo Jumatano Septemba 18, 2019 Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Dk James  Mataragio amesema mradi huo wa awali kwa Mtwara umegharimu Sh3.7 bilioni ikiwa ni fedha za ndani.

Amesema kwa mwaka wa fedha wa 2019/20 shirika hilo limepanga kuendelea na uunganishwaji wa wateja wapya 1,300 ambapo kati ya hao 310 ni wateja wa Mtwara kwa matumizi ya kupikia majumbani na taasisi mbalimbali na kwamba ni endelevu ambapo watakuwa wakitenga fedha kila mwaka kwaajili ya utekelezaji.

 

“Mteja atawekewa mita ya kupima kiasi cha gesi anayotumia kwa mwezi na hii inafanya kazi kama luku za umeme, mteja atatakiwa kununua unit za gesi ambazo atatumia zikiisha atanunua tena nyingine ambapo utaratibu huu unaitwa malipo kabla ya kutumia (pre-paid) kwa kutumia kadi maalum,” amesema Dk Mataragio

Pia Soma

Advertisement
Amesema matumizi ya familia ya watu sita inakadiriwa kuwa Sh29,000 ikiwa ni punguzo la asilimia 40 ikilinganishwa na vyanzo vingine vya nishati ambapo gharama hizo zilizokadiriwa kutoka kwa watumiaji wa Dar es Salaam walioanza kutumia gesi toka mwaka 2015 ambapo matumizi ya familia ya watu sita ni wastani wa nusu ya mitungi ya LG.

“Niwaondoe hofu wananchi kuhusu usalama wa matumizi ya gesi asilia kwa kuwa gesi hii ni salama zaidi ukilinganisha na gesi ya mitungi au mafuta ya taa.”

“Usalama huu unasababishwa na utabia yake (gesi) kwamba ni jepesi kuliko hewa tunayovuta hivyo kupotelea hewani mapema ikitokea imevuja na kuondoa uwezekano wa kulipuka na kusababisha moto,” amesema Dk Mataragio

Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani amesema ipo gesi ya kutosha na kwamba kwa sasa zipo futi za ujazo 57.54 trilioni ambazo zimetengwa katika matumizi mbalimbali kama uzalishaji wa umeme zimetengwa futi za ujazo 8.8 trilioni huku matumizi ya nyumbani yakitengewa futi za ujazo 1.20 trilioni kwa lengo la kumpunguzia gharama mtumiaji.

Amesema asilimia 55 ya umeme unaotumika nchini unatokana na rasilimali gesi.

Waziri huyo amesema zimetengwa futi za ujazo 4.35 trilioni kwa ajili ya matumizi ya viwanda vya mbolea na petroli chemicals na kwamba baadhi ya viwanda tayari vilishapewa kibali cha kutumia gesi ikiwemo cha saruji cha Dangote.

“Viwanda vingine vya kawaida vikubwa tumevitengea gesi futi za ujazo 3.65 trilioni kama Rorya na kwingineko na wiki ijayo nitakwenda kuwasha kiwanda kitakachotumia gesi Mkuranga, watumiaji tunataka watumie gesi,” amesema Dk Kalemani

Chanzo: mwananchi.co.tz