Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtanzania anayemiliki kiwanda kikubwa Thailand

Au.png Mtanzania anayemiliki kiwanda kikubwa Thailand

Tue, 3 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WAKATI wa ziara ya Ujumbe wa Tanzania nchini Thailand, mbali na kutembelea shughuli za madini, ulipata wasaa wa kukutana na kijana wa Kitanzania Suleiman Kilonda aliyewekeza jijini Bangkok nchini humo kwa kumiliki kiwanda cha kushona na kuchapisha fulana cha Sk Export.

Mbali na kumiliki kiwanda, Suleimani amefungua maduka ya kuuza nguo za aina mbalimbali zenye chapa zake za African Man, African Queen, Town Totoz na King Kaka ambapo ameajiri wafanyakazi wapatao 200.

Katika mahojiano maalum, Suleiman amesema malengo yake ni kufungua kiwanda kikubwa nchini Tanzania chenye uwezo wa kuajiri watanzania wengi na kutumika kama sehemu ya kujifunzia kwa kila mtanzania mwenye ndoto za kumiliki kiwanda cha nguo.

‘’Tayari nimeshanunua sehemu ya kufungua kiwanda nchini Tanzania katika eneo la Mlandizi ramani ninayo ya aina ya kiwanda ninachotaka kukifungua lakini changamoto bado natafuta fedha za kuanza ujenzi, nimejaribu kwenda kwenye baadhi ya taasisi za fedha lakini bado sijafanikiwa. Ombi langu langu kwa Serikali ni kuniwezesha kufikia ndoto hiyo ambayo itawasaidia na watanzania wenzangu kupitia mimi,’’ amesema Suleiman.

Ameongeza kuwa, malengo ni kujenga kiwanda chenye uwezo wa kuajiri watu 2,500 na uwezo wa kuzalisha nguo 100,000 kwa siku.

Kwa upande wake, Afisa Mipango Miji kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Michael Majebele amesema Mipango yake ya uwekezaji ni mzuri tija kwa taifa, kuanzia kwenye suala la ajira, kodi na kubadilishana ujuzi hivyo na kueleza kuwa, mwekezaji huyo anakaribishwa TIC ili aweze kusajili mradi wake jambo ambalo litamwezesha kufurahia vivutio vya uwekezaji vinavyotolewa nchini ambavyo vitamsaidia kwenye kupunguza gharama za uanzishaji wa kiwanda chake. -

Chanzo: www.tanzaniaweb.live