Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtandao wa Twitter wapata hitilafu, wapotea hewani

Twitter Wafuasi Mtandao wa Twitter wapata hitilafu, wapotea hewani

Thu, 14 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtqndao wa Kijamii wa Twitter, umepata hitilafu duniani kote mchana huu na kusababisha watumiaji wa mtandao huo washindwe kuingia.

Kutokana na hitilafu hiyo, watumiaji wote wenye akaunti katika mtandao huo, wametolewa nje (log out) na kuwafanya washindwe kuingia tena (log in), hali iliyozusha taharuki kubwa duniani kote.

Mtandao wa Down Detector unaoshughulikia kutambua na kuthibitisha matatizo ya kimtandao duniani kote, umeeleza kwamba watumiaji waliokuwa wa kwanza kupata madharta hayo ni katika majiji makubwa ya London na Birmingham nchini Uingereza na New York na Los Angeles nchini Marekani kabla ya madhara kusambaa duniani kote.

Hofu ya wengi ni kwamba huenda mtandao huo umedukuliwa ambapo jitihada za wataalamu wa teknolojia wanaendelea na kazi ya kudhibiti tatizo hilo na tayari mtandao huo umeanza kurejea kwenye baadhi ya maeneo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live