Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtaalamu atahadharisha kugeuka taifa la madalali

20906 Mtaalamu+pic%2527 TanzaniaWeb

Sat, 6 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mbia wa Kampuni ya KPMG, Alexandra Njombe amesema iwapo Watanzania hawatashirikishwa ipasavyo katika kujenga uchumi wa kati kupitia viwanda, kuna hatari ya kutengeneza taifa la madalali.

Hayo ameyasema leo Oktoba 4, 2018 katika mjadala wa Jukwa la Fikra la Mwananchi linalolenga kujadili fursa, changamoto na ufumbuzi kuelekea uchumi wa viwanda ambalo limeandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) na kurushwa moja kwa moja na televisheni ya ITV.

Amesema ili kuhakikisha kila mwananchi anashiriki lazima wapewe elimu ili wajue kiwanda ni nini, namna anavyoweza kushiriki na kutamani kumiliki badala ya kuwaachia watu wachache huku wengi wakiwa wasindikizaji.

"Tukifanya hivyo tutakuwa tumeweza kubadili fikra zao na kuwafanya watamani kujaribu katika kile alichokisoma na atamani kushiriki kujenga uchumi wa viwanda, siyo kuwaachia wengine," amesema Njombe.

Amesema miongoni mwa mambo yanayoweza kuchangia katika kujenga utayari wa ushiriki wa Watanzania ni kutazama upya mitalaa ya masomo kwa wanafunzi na kuangalia namna ya kupenyeza stadi za kazi ili waweze kujifunza kuanzia shuleni.

"Kufanya hivyo tutakuwa tumeongeza rasilimali watu na wataalamu wa kutosha ambao watatusaidia katika safari hii ya matumaini," amesema Njombe.

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz