Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msukuma: Hereni za ng'ombe zina faida zipi?

Hereni Ngombe.jpeg Msukuma: Hereni za ng'ombe zina faida zipi?

Wed, 3 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Jimbo la Geita Joseph Kasheku Musukuma amehoji Bungeni faida ya kuweka hereni kwenye ng’ombe na amemtaka Waziri wa Mifugo na Uvuvi kujinasua kwenye mtego huo.

Musukuma amesema hayo wakati akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi iliyoomba kiasi cha Shilingi 295,920,933,000. kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

“Mimi sipingani na maagizo ya Waziri mkuu tunaboresha hivi ng’ombe zikigombana kule poroni hereni ikadondoka mtaniambia anayepigana nae ni nani?, ng’ombe zangu zikiiibiwa zikapelekwa Mtwara mtanipigia Musukuma usiende Polisi fuata ziko Mtwara?, Waziri usiingie kwenye huu mtego sijui unanisikiliza au unachati?”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live