Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msitumie mawakala kwenye maduka ya kubadili fedha

Dola Dola Juu Juu Msitumie mawakala kwenye maduka ya kubadili fedha

Wed, 25 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wafanyabiashara ambao wanaomba lesseni za kufungua maduka ya kubadilisha fedha za kigeni Benki Kuu ya Tanzania (BoT), wametakiwa wasitumie madalali.

Ushauri huo umetolewa na maofisa wa BoT waliofika mkoani Kagera na kutoa ufafanuzi juu ya kanuni mpya za mwaka 2023 zilizofanyiwa marekebesho kutoka kanuni za mwaka 2019 kuhusu kufungua maduka na matawi ya kubadilishia fedha za kigeni.

Mkuu wa kitengo cha uchunguzi BoT, Amri Mbalilaki amesema kuwa kanuni za mwaka 2023 za kumiliki duka la kubadilisha fedha za kigeni zimepunguza mtiririko wa vikwazo vingi kwa Watanzania wazawa kupata leseni za umiliki, ukilinganisha na miaka ya nyuma, hivyo hakuna sababu kutumia dalali ambaye atachukua fedha nyingi kwa mfanyabiashara bila sababu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live