Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msitumie Malori kusafirisha Minofu- Waziri

6ca3e3d54e3512267eebdcfbb31e463e Msitumie Malori kusafirisha Minofu- Waziri

Tue, 5 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki amewataka wawekezaji wa viwanda vya samaki vilivyopo mkoani Mwanza kuhakikisha kuacha kutumia usafiri wa malori kusafirisha minofu na badala yake watumie usafiri wa ndege ili kutangaza bidhaa zinazotengezwa hapa Tanzania.

“Tungependa kuona usafirishaji wa minofu ya samaki unafanyika hapa nchini kwetu, badala ya nchi jirani kwa kusafirisha kwa malori kwenda nchi za jirani,” alisema na kuongeza

“Kuna uwekezekano kabisa wa kutoa minofu ya samaki kutoka kiwanja cha ndege cha Mwanza kwenda nje ya nchi badala ya kutumia nchi za jirani.” amefafanua Ndaki

Aidha, amewataka wawekezaji wa viwanda vya samaki kuangalia namna ya kuongeza bei ya kununulia samaki kwa wavuvi wanaopeleka samaki katika viwanda hivyo ili wavuvi hao waweze kubadilisha maisha yao na kunufaika kupitia Sekta ya Uvuvi.

Waziri Ndaki amebainisha hayo baada ya Meneja Mkuu wa Kiwanda cha kuchakata samaki cha Nile Perch Rupesh Mohan kumueleza Waziri Ndaki na Naibu Waziri Pauline Gekul kuwa viwanda vya samaki vimekuwa vikikosa malighafi ya kutosha kutokana na soko la ndani kukua na wakati mwingine kupata samaki kwa bei ya juu.

Akijibu changamoto hiyo Waziri Ndaki alisema kuwa kama bei ya soko la ndani imepanda ni dhahiri wavuvi watauza samaki katika soko hilo badala ya kupeleka viwandani ambapo wanauza kwa bei ndogo.

Amevitaka viwanda hivyo vya kuchakata samaki kuangalia upya bei ya samaki wanayonunua ili wavuvi nao waweze kunufaika na kuboresha maisha yao na viwanda pia viweze kupata malighafi za kutosha.

Chanzo: habarileo.co.tz