Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mshindi wa safari ya Disney Hong Kong kutoka GSM Mall apatikana

3627 DSC 6255 1 TZW

Mon, 26 Feb 2018 Chanzo: bongo5.com

Makazi wa Mbezi Beach jijini Dar es salaam Bi.Kosolata Mulebusi amejishindia safari ya kwenda Disney Hong Kong kwa hisani ya Maduka ya GSM Mall nchini.



Mmoja kati ya wateja wa GSM Mall akiokota karatasi ambayo ilimfanya mwanadada huyo atangazwe.

Kampuni ya GSM MALL imeanzisha shinda ambalo lilianza tangu mwezi Desemba mwaka jana hadi Tarehe 4Feb-mwaka huu ambapo wateja waliokuwa wakifanya manunuzi ya kuanzia Laki na Nusu (150000) walikuwa wakipewa Kuponi ambayo ilikuwa ikimpa nafasi Mnunuzi kujishindia Safari ya kuelekea Disney Hong Kong.



Meneja Masoko wa GSM MALL Farida Rubanza akizungumza na wandishi wa Habari wakati wa shindano hilo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam leo hii wakati wa uchezeshaji wa Droo hiyo katika Moja ya Duka hilo liliopo Mkabala na Oysterbay polisi jijini Dar es salaam, Meneja Masoko wa GSM MALL Bi. Farida Rubanza amemtangaza Mshindi wa shindalo hilo kuwa ni Bi.Consolata Mulebusi,Mkazi wa Mbezi Beach Jijini Dar es salaam.

Mshindi huyo ameeleza kwa njia ya simu kufurahishwa kwake na shindano hilo na kuwataka wananchi kununua bidhaa katika Maduka ya GSM MALL ili kujishindia nafasi hiyo.

Naye mmoja kati ya wanunuzi wa GSM MALL Bw.Edward Laurent Mkazi wa Mtwara ameishukuru kampuni hiyo kwa kuedesha shindano hilo na kuwapa Fursa wananchi kutembelea Hong Kong ikiwa ni moja ya sehemu ya utalii duniani.

“Mimi nimekuja kununua vitu hapa dukani nimetoka Mtwara nimekuja hapa Dar es Salaam kwa kazi zangu nimeitwa tu na wameniomba niokote ticket, kwanza huyu mshindi hata simfahamu, kwakweli nimeona shindano hili ni la haki na kweli nawaomba watu wote na wateja wa GSM kuendelea kutumia bidhaa zao hata mimi hapa nimekuja kununua bidhaa zao” Alisema Edward

Mshindi huyo ametakiwa kuwasili katika ofisi za GSM MALL ili kufuata taratibu za safari yake na Familia yake.

Chanzo: bongo5.com