Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mshindi wa Chemsha Bongo ya Tigo akabidhiwa gari lake

87310 CHEMSHA+PIC Mshindi wa Chemsha Bongo ya Tigo akabidhiwa gari lake

Fri, 6 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkazi wa Zanzibar, Shaban Khamis Ali (49) leo amekabidhiwa rasmi gari yake aina ya Renault Kwid yenye thamani ya Sh23 milioni baada ya kuibuka mshindi wa promosheni ya Tigo Chemsha Bongo 2019.

Promosheni hiyo iliyodumu kwa siku 90 kuanzia tarehe 4 Agosti hadi 14 Novemba 2019 iliwapa wateja nafasi ya  kujishindia zawadi za pesa taslim kila siku na droo ya mwisho mshindi alikuwa alijinyakulia zawadi ya gari.

“Wakati napigiwa simu,nilikuwa nyumbani najipanga kutoka kuenda katika mihangaiko yangu ya kibiashara, basi nilipopata ile taarifa kwamba nimeibuka mshindi nilifurahi sana kwani sikutegemea kabisa kuwa ningeibuka mshindi katika promosheni hii, habari hizi naziona kama ndoto kwangu,“ Shabani alisema kwa furaha. 

Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani, Joseph Mutalemwa, alimpongeza mshindi huyo na kutumia fursa hiyo kuwashukuru wateja wote wa kampuni ambao walishiriki na baadhi yao kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslimu ambayo yalitolewa na kampuni hiyo.  “Tunayo furaha kubwa katika kipindi hiki tunachoelekea katika msimu wa sikukuu kumkabidhi mshindi wetu wa gari ya aina Renault Kwid, gari hili ni jipya kabisa,. Tunawashukuru wateja wetu nchi nzima walioshiriki kwenye promosheni hii ya miezi mitatu ambayo imemalizika mwishoni mwa mwezi wa Novemba 2019”. alisema Mutalemwa. 

Aliongeza kuwa, promosheni hiyo ambayo ilianza jijini Mwanza katika msimu wa Tigo Fiesta 2019-Saizi Yako  imepata mafanikio makubwa kutokana na wateja wengi kujitokeza kushiriki na baadhi yao kufanikiwa kujishindia zawadi(fedha taslim) mbalimbali na hivyo Tigo kufanikisha lengo lake ambalo lilikuwa ni kuwashukuru wateja kwa kuiunga mkono kampuni kupitia kununua bidhaa zake mbalimbali. 

Chanzo: mwananchi.co.tz