Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mradi waongeza fursa za ajira, ukuaji uchumi

D4f88c9e50f9338e1b5be863306b2bdf Mradi waongeza fursa za ajira, ukuaji uchumi

Tue, 13 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MRADI wa upanuzi unaoendelea unaolenga kuongeza uwezo wa kuhifadhi mafuta ya gesi ya magari utaiwezesha kampuni Sahara Tanzania kuwa moja ya vituo vikubwa zaidi vya uhifadhi huku ikiongeza fursa za ajira na ukuaji uchumi nchini; Imeelezwa.

Meneja wa kampuni Sahara Limited Tanzania, Olumuyiwa Aladejana, alisema katika taarifa yake kuwa, kampuni inao mradi wa upanuzi unaolenga kuongeza uwezo wa kuhifadhi mafuta ya gesi ya magari nchini.

Kwa mujibu wa Aladejana, kampuni imepanua eneo lake la kuhifadhia mafuta ya petroli hadi kufikia lita milioni 72 sambamba na kujitolea kukuza upatikanaji wa bidhaa nchini na katika nchi nyingine za Afrika.

“Sahara imeongeza na kupanua miundominu yake kutoka vifaa vya kupakia mizigo 10 na maeneo manne ya kuhifadhia mafuta yenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni 36 hadi vifaa 20 vya kupakia mizigo na maeneo nane ya hifadhi ya mafuta yenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni 72 za mafuta,” alisema.

Aladejana alisema hatua hiyo imesaidia kuchochea maendeleo ya uchumi nchini Tanzania kupitia upatikanaji wa bidhaa za mafuta.

Akizungumza na wachambuzi wa vyombo vya habari kuhusu utendaji wa kampuni hiyo, Aladejana alisema walifurahishwa na fursa hiyo ya kuunga mkono Dira ya Taifa ya 2025.

“Dira ya 2025 inawakilisha maono mapana ya malengo ya maendeleo ya Tanzania kama nchi ya kipato cha kati, inayolenga maisha bora, amani, utulivu na umoja; utawala bora; jamii yenye elimu na uchumi wa ushindani wenye uwezo wa ukuaji endelevu na faida za pamoja,” alisema.

Akaongeza: “Sahara Tanzania imejitolea kuchangia kufanikisha lengo hili zuri kupitia shughuli zetu katika sekta ya nishati na hatua kwa njia ya miradi ya maendeleo endelevu nchini.”

Alizipongeza sera thabiti za serikali ya Tanzania na kusisitiza kuwa, kampuni hiyo itaendelea kushirikiana na wadau wote kufanikisha azima hiyo. Hata hivyo, alibainisha kuwa nchi za Kiafrika zinahitaji kuoanisha vipimo vya bidhaa zao ili kukuza shughuli za ndani ya Afrika.

“Tunaona ulimwengu ukielekea kwenye mafuta safi na kiwango kidogo cha kaboni na Sulphur. Uainishaji uliowekwa unarahisisha mtiririko rahisi wa bidhaa katika maeneo yote ya Afrika, mwishowe kuifanya Afrika iwe na ushindani zaidi,” alisema.

Mtendaji wa Maendeleo ya Biashara kutoka Sahara Tanzania Limited Mwajabu Mrutu, alisema kushiriki kwa Sahara Tanzania kuleta fadhila kwa taifa kumewekwa katika mipango yake ya uraia wa ushirika.

Mrutu alisema hatua za Sahara Tanzania ni pamoja na kuboresha maktaba katika Shule ya Sekondari ya Pugu inayohudumia zaidi ya wanafunzi 1,000 na utoaji wa vyoo na vyumba vya kuoshea katika Shule ya Sekondari ya Salma Kikwete ili kukuza lengo la Maendeleo Endelevu linalozungumzia usafi na usafi wa mazingira.

Chanzo: www.habarileo.co.tz