Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mradi wa gesi Songosongo uko vizuri

Nishati Songo Mitambo ya uchakataji gesi Songosongo

Mon, 4 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali ametembelea na kukagua miundombinu ya Mradi wa kuzalisha na kuchakata Gesi asilia wa Songosongo uliopo Mkoani Lindi.

Mahimbali amesema kuwa lengo la ziara hiyo iliyofanyika Machi 31, 2022 ni kutaka kuona shughuli za uzalishaji, uchakataji na usafirishaji wa Gesi asilia kutoka katika visima vya Gesi vilivyopo katika eneo la bahari nan chi kavu katika eneo hilo.

Katika ziara hiyo ametembelea mitambo ya kuchakata gesi asilia ya Songosongo, eneo ililofungwa mtambo mpya wa kuongeza mgandamizo wa Gesi asilia, pamoja na Kisima namba kumi (10) kinachofanyiwa ukarabati.

Aidha alitembelea kisima namba nne (4),(12), 11 pamoja na sehemu ambayo gesi inayozalishwa kutoka visimani inasafirishwa kuingia katika bomba la kusafirisha Gesi asilia kwenda Somangafungu hadi Kinyerezi, Dar es salaam kwa ajili ya kuzalisha Umeme na matumizi mengine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live