Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mradi wa bomba la mafuta waanza kulipa

Bomba La Mafuta Msh Mradi wa bomba la mafuta waanza kulipa

Mon, 18 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Imeelezwa kuwa mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga (EACOP) umeanza kuleta faida kupitia kodi mbalimbali zinazofikia takribani shilingi bilioni 30 na kuzalisha ajira kwa Watanzania.

Akiongea na vyombo vya habari, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Deus Sangu amesema kamati imejiridhisha na maendeleo ya mradi ambao unajengwa na kuwa na matarajio makubwa katika kuchangia kwenye uchumi wa Taifa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Balozi Omben Sefue, amewahimiza Watanzania kuchangamkia fursa za mradi huo ikiwemo ajira.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mussa Makame amesema kuwa ushirikishwaji kwa wananchi upo wa kutosha katika kila hatua ya ujenzi wa mradi huo.

Serikali ya Uganga na Tanzania zimekubaliana kujenga Mradi huu wa kimkakati wenye kilomita 1,445 ambapo kwa Tanzania pekee kuna kilometa 1,147. Mpaka kukamilika mradi unatazamiwa kugharimu Dola za Marekani bilioni 5.1 (takribani shilingi trilioni 11).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live