Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mradi wa SGR kuongeza ufanisi wa biashara

Tanzania SGR.png Mradi wa SGR kuongeza ufanisi wa biashara

Fri, 4 Nov 2022 Chanzo: eatv.tv

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amesema kutekelezwa kwa mradi wa Reli ya kisasa (SGR) kutoka Uvinza mkoani Kigoma nchini Tanzania hadi Kindu DRC kupitia Gitega nchini Burundi kutaongeza ufanisi katika matumizi ya Ukanda huru wa biashara Barani Afrika.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati akiongoza majadiliano na wawekezaji kuhusu mradi wa reli hiyo ya kisasa, majadiliano yaliofanyika katika Jukwaa la Uwekezaji Barani Afrika linalofanyika Jijini Abidjan nchini Ivory Coast. 

Amesema serikali zote tatu zimeweka nia ya dhati ya kutekeleza mradi huo ambapo kwa upande wa Tanzania tayari imekwisha tekeleza miradi unganishi ya reli ya kisasa inayochagiza uwepo wa mradi huo muhimu.

Aidha Makamu wa Rais amesema asilimia 50 ya mizigo inayotoka katika bandari za Tanzania hupelekwa nchi za Burundi na Kongo hivyo uhitaji wa reli hiyo ya kisasa ni muhimu kwa sasa. 

Kwa Upande wake Waziri wa Miundombinu wa Burundi Mh. Dukundane Dieudonneè amesema taifa hilo limekuwa likipoteza zaidi ya dola za marekani milioni 17 kila mwaka katika usafirishaji wa mizigo hivyo mradi huo utasaidia katika kubaliana na hali hiyo. 

Awali katibu mtendaji wa sekretarieti ya eneo huru la biashara barani Afrika Wamkele Mene amesema ufanyaji biashara baina ya nchi za Afrika umekua na changamoto na gharama kubwa kutokana na kutokuwepo na miundombinu rafiki.

Katika majadiliano hayo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa amewasilisha mipango ya utekelezaji wa mradi huo kwa wawekezaji mbalimbali na kueleza mafanikio yaliopatikana katika utekelezaji wa miradi ya awali ya Reli ya Kisasa nchini Tanzania.  

Chanzo: eatv.tv