Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mradi wa REGROW watoa ajira 178

Regrow Kusini (600 X 380) Mradi wa REGROW watoa ajira 178

Mon, 30 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mhandisi Mkazi wa Mradi wa Kuendeleza Maliasili na Kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW) kwa upande wa majengo, Mhando Jambia amesema, mradi huo umetoa ajira 178 kwa Watanzania katika maeneo mbalimbali katika Hifadhi ya Taifa ya Nyerere kunakofanyika mradi huo.

Kati ya ajira hizo, 78 ni za kudumu mpaka mwisho wa mradi huo ambao umeanza Mei 10, 2023 hadi Agosti 13, 2024 na ajira 100 ni za muda mfupi mfupi kulingana na mahitaji ya watu katika sehemu ya kazi za mradi huu.

Mradi huo unahusisha ujenzi wa majengo ya wafanyakazi wa Hifadhi ya Taifa ya Nyerere, kempu za watalii, geti la kuingia na kutokea mbugani Mtemere na nyumba za kulala watalii.

Mhandisi Jambia ameyasema hayo wakati akizungumza na wanahabari kuhusu tathmini ya utekelezaji wa mradi wa REGROW katika hifadhi hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live