Serikali imesema hadi kufikia Mei 15, 2023 mradi wa ujenzi wa mradi wa Morocco Square unaosimamiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ulikuwa umekamilika kwa asilimia 100.
Serikali imesema hadi kufikia Mei 15, 2023 mradi wa ujenzi wa mradi wa Morocco Square unaosimamiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ulikuwa umekamilika kwa asilimia 100. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula ameliambia Bunge jijini Dodoma kuwa miradi mingine ya Kawe 711 na Golden Premium Residence mazungumzo kati ya NHC na Wakandarasi yanaendelea ili kazi iweze kuendelea na kwa mradi wa PLOT 300 Regent Estate haukutekelezwa kutokana na fedha iliyokuwa imetengwa kuhamishiwa katika mradi wa nyumba za gharama nafuu wa Samia Housing Scheme uliopo Kawe.