Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mradi wa Café Africa waongeza uzalishaji wa kahawa

Ce1e1d1de24ba9a3d55c28cff811d969 Mradi wa Café Africa waongeza uzalishaji wa kahawa

Fri, 18 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MRADI wa kuongeza uzalishaji wa kahawa mkoani Kagera utakaomalizika mwaka 2024 umefikia tamati katika awamu ya kwanza, baada ya kuhitimisha kwa mafunzo ya maofisa ugani na wakulima wa kahawa 200.

Mradi huo unafadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Cafe Africa.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Marco Gaguti akifunga awamu wa kwanza ya utekelezaji alisema kuwa kuwepo wa mradi huo kumefanikisha mkoa wa Kagera kuvuna tani za kahawa zipatazo 72,000.

Akitoa taarifa ya mavuno ya kahawa mkoani Kagera alisema mwaka 2017/2018 mkoa ulipata tani 52,000, mwaka 2018/2019 ulivuna tani 58,000 na mwaka 2019/2020 baada ya Cafe Africa kwa kushirikiana na Bodi ya Kahawa mkoa wa Kagera ulipanga kupata tani za kahawa 60,000 lakini zimepatikana 72,000.

Alisema mradi huo utakapofika ukingoni mkoa wa Kagera utaendelea kuwa kinara kwa kuwawezesha wakulima kulima kilimo chenye tija ambacho kinatumia nguvu kidogo lakini kinatoa mavuno mengi.

Akitaja moja ya hatua kubwa ya utekelezaji wa mradi wa Cafe Africa ni kutambua nguvu ya vijana ambapo pamoja na wakulima na maofisa ugani kuhitimu mafunzo ya kilimo cha ufufuaji na uzalishaji kahawa vijana 40 wamehitimu.

Alisema lengo ni kuhamasisha kilimo cha kahawa kwa vijana wenzao na kuanzisha maduka /migahawa ya kunywa kahawa katika vijiji vyao jambo litakaloongeza thamani ya kahawa na ajira vijijini.

Mratibu wa Cafe Africa mkoani Kagera, Daniel Mwakalinga alisema mradi huo uligawanyika katika makundi matatu, ambayo ni utoaji elimu kwa maofisa ugani ambapo 168 wamepata elimu ya kutosha ya zao la kahawa, kufufua miche ya mibuni iliyochoka, kuotesha miche mipya ili kuendelea kuwagawia wakulima bure.

Kwa mujibu wa Katibu Tawala wa mkoa wa Kagera, Profesa Faustine Kamuzola ambaye mara nyingi anasema kuwa amesoma mpaka juu kutokana na zao la kahawa, alisema mkoa wa Kagera unaweza kuzalisha hadi kufikia tani za maganda 200,000 ifikapo mwaka 2025.

Mtafiti mwandamizi kutoka taasisi ya utafiti wa zao la kahawa TACRI, Dk Nyabisi Nghoma alisema mkoa wa Kagera unapoteza tani za kahawa safi zipatazo 39,000 kutokana na wakulima kulima kilimo kisicho na tija na baadhi ya wakulima kushindwa kubadilika kwa kushikilia mibuni ya zamani.

Chanzo: habarileo.co.tz