Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi amesema utekelezaji wa ujenzi wa Mradi wa Maji Butimba unakwenda vizuri na sasa umefikia asilimia 96 na unatarajia kuanza majaribio mwishoni mwa wiki hii.
Makilagi amesema hayo leo Septemba 12, 2023 akiwa ameambatana na Kamati ya ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Nyamagana sambamba na Menejimenti ya Mwauwasa ikiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Neli Msuya kwaajili ya kujionea maendeleo ya ujenzi wa mradi huo kabla ya kukamilika kwakwe na kuanza majaribio.
"Niwapongeze MWAUWASA kwa kazi nzuri na kasi hii ya utekelezaji mnayoendelea nayo niipongeze pia timu iliyoundwa na Waziri wa Maji Jumaa Aweso, kwa ushirikiano huu mnaotoa kwa MWAUWASA, tuna imani tutapata matokeo chanya,"
Imeandaliwa na Cyprian Magupa Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) Neli Msuya amesema utekelezaji wa mradi huo wa Butimba sasa umefikia asilimia 96 ikiwa ni hatua ya awali kuelekea katika hatua ya ukamilishwaji. -
Inaelezwa kuwa kukamilika kwa Mradi wa Maji Butimba kutaenda kutatua kero na changamoto ya upatikanaji wa maji safi katika Jiji la mwanza na maeneo ya jirani ambapo mradi huo unatekelezwa kwa gharama ya ya Shilingi.Bilioni 69 na unatarajia kuzalisha kiasi cha Lita Milioni 48 kwa siku na utahudumia zaidi ya wakazi 450,000.