Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mradi wa BBT kubisha hodi Rufiji

Kilimo House Mradi wa BBT kubisha hodi Rufiji

Wed, 20 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Samia Suluhu Hassan, akiwa njiani kurudi Dar es Salaam, baada ya kumaliza ziara yake katika mikoa wa kusini, alisimama kwa muda kusalimia wakazi wa Rufiji, huku akiwataka vijana kuingia katika mradi wa BBT – Kujenga Kesho Bora ya Vijana, mradi ambao utarajia kuanza hivi karibuni.

“Rufiji hapa kama mnavyojua tuna bonde kubwa sana la Rufiji, ambalo robo yake tumechukua na kujenga bwawa la kubwa la umeme, lakini eneo lilibaki linakwenda kuwa la kilimo. Sasa zile nika kama hekta nyingi, zaidi ya 60, 000,” amesema na kuongeza;

“Lakini tunakwenda kuweka skimu ya umwagiliaji, na kuanzia mwaka huu, tunakwenda kujenga umwagiliaji maji kwa hekta 3000, na tutakuwa tunaendeleza hivyo kila mwaka, ili wananchi mbali na ufuta, korosho, na mbaazi, muweze kuzalisha mpunga.”

Rais Samia amesema kuwa dunia inabadalika, na hivyo mpunga sasa ni zao la bishara na kwamba antaka Rufiji itambuliwe duniani kutokana na kuzalisha kwa wingin zao hilo na kuliuza nje.

“Nani alijua mbaazi leo itakuwa zao la biashara, tulijua mbaazi ni mboga tu, lakini leo ni zao la biashara. Kwa hiyo na mpunga nao ni zao la biashara, Tanzania tunauza mpunga mpaka Ulaya, sasa niwaombe sana tunakuja kujenga umwagiliaji maji, ingieni na hasa vijana,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live