Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mradi mwendokasi Mbagala- Gerezani wafikia asilimia 60

503f42a92b84925d0e5798b7a566405a.jpeg Mradi mwendokasi Mbagala- Gerezani wafikia asilimia 60

Tue, 28 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart) kutoka Mbagala hadi Gerezani, Dar es Salaam umekamilika kwa asilimia 60. Mkurugenzi wa Fedha na Maendeleo ya Biashara Dart, Deusdelity Casmir alisema hayo jana wakati wa uzinduzi wa safari za mabasi hayo kutoka Mbagala Rangi Tatu hadi Viwanja vya Sabasaba katika Barabara za Kilwa.

“Leo (jana) tumeizundua njia ya mradi wa mabasi yaendayo haraka kutoka Mbagala Rangi Tatu hadi Viwanja vya Sabasaba ndani lengo likiwa ni kuwarahisishia usafiri abiria ambao wanahitaji kwenda Viwanja vya Sabasaba kwa ajili ya maonesho ambayo yanaanza, hivyo basi uzinduzi huu ni sehemu ya majaribio yatakayodumu kwa siku 16 na baada ya maonesho huduma itasitishwa,” alisema Casmir.

Alisema asilimia 40 za ujenzi wa mradi huo zilizobaki zitakamilika Machi, 2023 kukabidhiwa serikalini. Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo aliwataka wananchi wawe na imani na serikali.

“Nipende kuwaambia wananchi kuwa wasiwe na wasiwasi na serikali, kwani Rais Samia Suluhu Hassan amedhamiria kumaliza miradi yote ya kimkakati na tulichokifanya leo nikuhakikisha usafiri kuelekea Viwanja vya Sabasaba unakuwa mzuri ikilinganishwa na miaka ya nyuma ambapo uligubikwa na foleni,” alisema.

HabariLEO jana lilishuhudia wakazi wa Mbagala wakipanda katika mabasi hayo hadi Viwanja vya Sabasaba na kisha mabasi hayo kuwapeleka eneo la Gerezani, Kariakoo. Kwa kuanzia, Dart imeanza na mabasi saba yatakayoanza safari saa 3:00 asubuhi hadi saa 2:00 usiku kuanzia jana hadi Julai 13, mwaka huu kwa nauli ya Sh 650

Chanzo: www.tanzaniaweb.live