Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mradi gesi asilia wapamba moto

Db08402c289c9a4435fe7c3bb99bcd49 Mradi gesi asilia wapamba moto

Thu, 28 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Serikali ya Majadiliano ya Mradi wa kusindika gesi asilia na kuwa hali ya kimiminika (LNG), leo imefanya ziara ya kutembelea eneo linalozalishwa gesi asilia la Mnazi Bay na kiwanda cha kuchakata gesi cha Madimba, Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara.

Akizungumza baada ya kutembelea miradi hiyo, mhandisi wa masuala ya mafuta na petrol, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Timu ya LNG, Charles Sangweni, amesema wajumbe wote wameridhishwa na kazi inayofanyika katika mitambo hiyo, kuanzia kwenye uzalishaji mpaka uchakataji.

Amesema mradi wa LNG ujenzi wake huchukua takriban miaka mine, mpaka mitano na mategemeo ni baada ya kukamilika majadiliano na wadau, pamoja kutafuta fedha za ujenzi huo, utaanza kutekelezwa, ambapo takribani Watanzania 5,000 watapata ajira.

Baadhi ya wajumbe wa timu hiyo, wamesema lengo la ziara yao ni kutaka kujua namna viwanda vinavyofanya kazi pamoja na mchakato mzima wa uendeshwaji wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live