Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mradi bomba la mafuta unavyomwaga ajira

Bomba La Mafuta Msh Mradi bomba la mafuta unavyomwaga ajira

Wed, 20 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imesema mradi wa bomba la mafuta ghafi kwa upande wa Tanzania umepunguza umaskini kwa kuwapatia vijana ajira na kuwajengea nyumba nzuri ambazo awali kabla ya kuhamishwa hawakuwa nazo.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Japhet Hasunga ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Vwawa amesema hayo leo walipotembelea mradi huo wa kupozea mafuta ghafi uliopo kijiji cha Sojo kata ya Ugusile Wilaya ya Nzega mkoani Tabora.

Hasunga amesema malengo ya kamati kutembelea mradi huo ni kuona fedha za umma zilizoidhinishwa na Bunge zimetekelezwa ipasavyo na kuendana na thamani ya mradi.

Hasunga amesema katika kuzungukia kiwanda cha kupozea mafuta ghafi amesema wamerizika kwa kuona Ila mahojiano zaidi yatafanyika siku zijazo bungeni.

“Kazi yetu kubwa tumekuja kuona na tumejionea uwekezaji huu imekuwa na tija kiasi gani na umekuja kukabiliana na umasikini kwa watu wetu,”amesema Hasunga.

Hasunga amesema baada ya kamati kuidhinisha fedha hizo utaratibu uliopo Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) unabaki kuwa na hicho la kumulika na kuleta ripoti lakini kilichowafurahisha mpaka sasa ni wananchi kulipwa fidia vizuri za fedha na kujengewa nyumba. -

Chanzo: www.tanzaniaweb.live