Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mradi DMP awamu ya pili kuanza

Lami Barabaraaaa Mradi DMP awamu ya pili kuanza

Thu, 24 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MRADI wa Uendelezaji Dar es Salaam (DMDP) umeingia awamu ya pili ya utekelezaji wake ukilenga kujenga barabara itakayoanzia eneo la Banana Ukonga hadi Hospitali ya Manispaa ya Ilala iliyopo Kivule Kitunda.

Hayo yamebainishwa na Ofisa Maendeleo wa mradi huo upande wa Ilala, Denis Mapembe alipozungumza na HabariLEO, Dar es Salaam jana na kubainisha kuwa barabara hiyo itakayojengwa kwa kiwango cha lami itakuwa na urefu wa kilometa 13 na upana wa meta 12.

“Kwa sasa tunaanza awamu ya pili ya DMDP tulishajenga barabara zote za Sinza katika awamu ya kwanza kwa hiyo kipande cha kwanza katika awamu ya pili ya mradi ndio hiki kipande cha Banana hadi Kitunda kitakuwa ni cha kiwango cha lami na kitawekwa taa, madaraja, mifereji, stendi za mabasi pamoja na alama zote unazozijua za barabarani,” alisema. - Alisema awamu ya kwanza ya ujenzi wa barabara hiyo itakuwa ni asilimia 30 huku asilimia 70 zilizobakia zitaenda kujadiliwa baadaye na kueleza kuwa kwa tathmini waliyoifanya wamejiridhisha katika awamu hiyo ya kwanza hakuna mtu yeyote atakayelipwa fidia.

Pia, alibainisha kuwa katika hatua za utekelezaji wa mradi itaundwa kamati ya malalamiko kuanzia ngazi ya mtaa hadi kata itakayokuwa na kazi ya kusikiliza changamoto mbalimbali zitakazojitokeza.

“Kamati itaundwa na wenyeviti wa mtaa barabara itakapopita, kusikiliza malalamiko na wahusika watakuwa wananchi wenyewe wataeleza kila kitu kuanzia ngazi ya chini kupanda hadi ngazi ya juu kama mtu kulalamika nyumba yangu imeharibika sijalipwa fidia au wakiona eneo fulani halijajengwa vizuri,” alibainisha.

Katika hatua nyingine Mapembe alisema kuwa shughuli rasmi za ujenzi zitaanza Aprili mwakani na wanategemea itakamilika ndani ya miezi 18 sawa na miaka miwili kwa awamu zote za mradi kwa ufadhili wa Benki ya Dunia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live