Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpango wa uendelezaji viwanda vidogo, kati rasmi

5114 Jenista Mhgm Mpango wa uendelezaji viwanda vidogo, kati rasmi

Mon, 13 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, amezindua mpango wa uendelezaji wa viwanda vidogo na vya kati ili kuwawezesha kiuchumi wajasiriamali wadogo na wa kati.?

Hatua hiyo inalenga kutatua tatizo la upatikanaji wa ujuzi, masoko na mitaji.?Akizindua mpango huo, Waziri Mhagama alisema utasaidia kuongeza kasi ya ujenzi na ukuaji wa uchumi kwa kutengeneza mazingira wezeshi na kuandaa mazingira yenye mfumo wa kibiashara itakayorahisisha kutengeneza uzalishaji wenye tija.?

Alisema mpango umejikita katika kuhakikisha kuwa wajasiriamali wanasaidiwa kuongeza ujuzi na kuhimili ushindani katika masoko ya ndani na nje.

?"Pia kuwezesha viwanda kupata vifaa vya kisasa kama mitambo kwa ajili ya kuongeza uzalishaji ili uwe na tija, kutoa mikopo yenye riba nafuu ili kupanua shughuli za uzalishaji pamoja na kuongeza kinga za hifadhi za jamii kwa wajasiriamali," alisema.?

Aidha, alisema kwa kupitia mpango huo wenye viwanda na wajasiriamali wamepewa fursa ya kupata mitaji, hivyo kutengeneza fursa za ajira kwa vijana wengi wanaohitimu vyuo katika ngazi mbalimbali.?Alifafanua sekta ya viwanda imeendelea kuwa na tija katika kuchangia ongezeko la pato la Taifa kwa kuongezeka kwa viwanda vidogo, vya kati na vikubwa.

?"Sekta ya viwanda katika pato la Taifa kwa mwaka 2019 ilikuwa asilimia 8.5 ikilinganishwa na asilimia 8.05 mwaka 2018, sawa na ongezeko la asilimia 0.45 na hii ni matokeo ya kuongezeka kwa shughuli za uzalishaji viwandani katika kipindi hicho," alisema.?

Naye Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa, alisema mpango huo umesadifu mikakati ya nchi katika uendelezaji viwanda na imekuja wakati mwafaka.?Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa, alisema mpango umeainisha namna bora ya kuwawezesha wananchi kiuchumi ikiwamo la kukuza mitaji na kuimarisha vyanzo vyao vya mapato na kukuza akiba na mikopo.?

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii(NSSF), William Erio, alisema mfuko huo umetoa Sh. bilioni tano kwa ajili ya utoaji mikopo kwa wajasiriamali hao wenye viwanda wanaojishughulisha katika kuzalisha bidhaa ili kuongeza mnyororo wa thamani.?

"Tupo taasisi nne ambapo NEEC ndio msimamizi wetu, pia kuna SIDO na VETA ambazo zinahusika na utambuzi wa miradi na utoaji wa mafunzo, sisi tumeshatoa Sh. bilioni tano ambazo zipo kwenye Benki ya Azania na zitaendelea kutolewa kulingana na uhitaji," alisema.?Alitoa wito kwa wajasiriamali kuchangamkia fursa hiyo kwa kuandaa maandiko ya kuomba fedha hizo huku akiwataka kuzitumia kwa malengo watakayoainisha kwenye maombi yao na si vinginevyo.?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live