Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpango wa maendeleo wataka ndege 19 kwa ATCL

B6cace57965deab6b392e8f3bc8f3298 Mpango wa maendeleo wataka ndege 19 kwa ATCL

Sun, 4 Jul 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MPANGO wa tatu wa Maendeleo ya Taifa wa miaka mitano (2021/22–2025/26, umelenga ifikapo mwaka 2026, Tanzania iwe imenunua jumla ya ndege 19 kwa ajili ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).

Kwa sasa, shirika lina jumla ya ndege nane huku ndege tatu zikitarajiwa kuingizwa nchini mwaka huu na kukamilisha idadi ya ndege 11. Pia serikali inatarajia kununua ndege nyingine ya mizigo.

Mpango huo uliozinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa hivi karibuni jijini Dodoma, unaonesha kutaongezwa idadi ya ndege za abiria za masafa marefu kutoka mbili zilizonunuliwa hadi tatu na kuongeza idadi ya ndege za masafa ya kati kutoka mbili zilizopo hadi nane ifikapo mwaka huo 2026.

Katika eneo la miundombinu ya sekta ya anga, mpango unaonesha idadi ya viwanja vya ndege vyenye taa za kuongozea ndege itaongezeka kutoka vinne hadi 10.

Viwanja vya ndege vyenye mifumo ya usimamizi wa taarifa za viwanja vya ndege, vitaongezeka kutoka kimoja kilichopo sasa hadi viwanja 14.

Chini ya mpango huo, idadi ya viwanja vya ndege vyenye mifumo ya usimamizi wa taarifa za viwanja vya ndege vitaongezeka kutoka 46 hadi 71.

Idadi ya viwanja vya ndege vyenye uzio kuzunguka kiwanja navyo vitaongezekwa kwa mujibu wa mpango huo kutoka viwanja tisa vya sasa hadi 27. Idadi za rada zitaongezeka kutoka tano za sasa hadi saba.

Kuhusu ndege tatu zinazosubiriwa kukamilisha ndege 11, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk Leonard Chamuriho, alisema serikali ya Awamu ya Sita imejipanga ndege mbili kubwa zitawasili kuanzia Septemba na moja Novemba na nyingine aina ya Bombardier inatarajiwa kuwasili nchini wakati wowote kuanzia sasa kwani ilichelewa kuwasili kutokana na janga Covid 19.

Akizungumza juzi kwenye kipindi cha siku 100 za Rais Samia Suluhu Hassan akiwa madarakani kilichorushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Chamuriho alisema serikali itaboresha viwanja vya ndege na kujenga vipya ikiwemo kiwanja cha ndege cha Msalato ambacho Rais Samia ameshatoa fedha kwa ajili ya kulipa fidia.

Alisema viwanja vingine vinafanyiwa ukarabati kwa ajili ya kuwekewa taa vifanye kazi saa 24 . Navyo ni Mwanza, Songwe, Mbeya na Iringa.

Kuhusu rada, alisema kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Anga Tanzania (TCIA), inadhibiti rada nne, moja Dar es Salaam, uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA), Mwanza na Songwe.

Chanzo: www.habarileo.co.tz