Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpango mkakati kuelekea Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati 2025

93511 Pic+viwanda Mpango mkakati kuelekea Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati 2025

Wed, 29 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

IMELEEZWA kuwa mipango thabiti kati ya serikali, sekta binafsi pamoja na kushirikiana na mitandao ya mawasiliano ya simu itasaidia kuhakikisha Tanzania inafikia uchumi wa kati na kuwa nchi ya viwanja ifikapo 2025.

Hayo yamo katika ripoti ya mwaka 2019 ya Kampuni ya ushauri wa mawasiliano ulimwenguni (GSMA) kwa serikali pamoja na mitandao ya mawasiliano ambapo katika ripoti hiyo imesema sekta ya mawasiliano ya simu ni muhimu katika kuhakikisha kufikia 2025 Tanzania inakuwa nchi ya viwanda na kufikia uchumi wa kati.

Ripoti hiyo ambayo inapatikana kwenye mtandao wa GSMA https://www.gsmaintelligence.com/ imesema mikakati ya kuifikisha Tanzania katika hali hiyo ilianza mwanzoni mwa karne hii ya 21 na kwamba inatambulika ni moja ya malengo makubwa ya Rais Dkt John Magufuli na serikali yake.

Ripoti hiyo imeendela kusema ili Tanzania ifike huko ni lazima nchi iwe na amani, kuondoa rushwa na kuwawekea wawekezaji na sekta binafsi mazingira bora na mazuri ya kufanya kazi. Ripoti hiyo imeongeza kuwa hadi sasa sekta nyingi nchini zimefaidika na uwekezaji, huku ikitoa mfano wa sekta ya mawasiliano ya simu ambayo kwa pamoja imeelezwa imewekeza zaidi ya shilingi trilioni 6 za Kitanzania hapa nchini.

Ripoti imeendelea kusema faida zingine zilizoletwa na uwekezaji huo mkubwa ni maisha ya watu yamebadilika na kuwa bora, mawasiliano mazuri, huduma ya kutuma na kupokea fedha pamoja na uwezo mkubwa wa matumizi ya internet na data. 

Ripoti hiyo inapendekeza kuwa ili kuendelea kuona faida za sekta binafsi ikiwekeza katika uchumi wetu lazima kuendelea kuhakikisha mazingira ya uwekezaji yanabaki bora kwa wawekezaji wa sasa na wajao. Hii italihakikishia taifa mazingira bora ya kuendelea kuvuna faida za uwekezaji na Watanzania kuendelea kufurahia matunda yake.

Pia Soma

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz