Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpango miaka 10 uchumi wa kidigitali waja

NAPE Mojaa.jpeg Mpango miaka 10 uchumi wa kidigitali waja

Tue, 20 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari iko katika hatua za mwisho katika hatua za mwisho kutoa mpango wa miaka 10 wa uchumi wa kidijitali utakaoonyesha ushiriki wa kila sekta katika kujenga uchumi huo.

Ameyasema hayo leo Jumanne ya Juni 20 katika Mwananchi Jukwaa la Fikra linalojafili mada isemayo Uwekezaji katika mabadiliko ya Kidigitali kwa ajili ya ustawi na ushirikishwaji wa jamii Dira 2025.

Akizungumza katika kongamno hiko, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema kupitia mpango huo Serikali itaendelea kujenga na kuwezesha miundombinu ya tehama.

"Mpango huu utakuwa ni kati ya mwaka 2023 hadi mwaka 2033, katika hili tunatamani kila mmoja afaidike twende pamoja tusimuache mtu nyuma tukiamini ushirikiano huu wa sekta binafsi na serikali wote tukishikamana oamoja inawezekana tukafanikiwa," anesema Nape.

Amesema kama waziri amekuwa akijisikia vibaya pindi anaposikikiza mijadala mbalimbali na kusikia kuwa mifumo ya kitanzania haisomani huku akieleza kuwa ni lazima kupiga hatua katika sehemu hiyo.

Alitumia nafasi hiyo kuutaka umma kuandaa mijadala kama hii kabla ya Serikali kufanya maamuzi.

"Changamoto ni kuwa, mijadala kama hii inakuja kipindi ambacho wafanya maamuzi wapo kwenye hatua za mwisho za kufanya maamuzi. Ni muhimu kuangalia ratiba za maamuzi za Serikali halafu hii mijadala itengenezwe," amesema.

Waziri huyo pia amesema ndani ya miezi mitatu au sita ijayo Serikali imelenga kuzindua mwongozo wa matumizi bora ya Tehama, sera ya miradi inayoanza (Start-ups).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live