Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpango kabambe wa mifugo kugharimu Sh1.39 bilioni

Mpango kabambe wa mifugo kugharimu Sh1.39 bilioni

Mon, 11 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Serikali imezindua mpango kabambe wa mifugo unaogharimu zaidi ya Sh1.39 bilioni.

Mpango huo umezinduliwa leo Machi 10, 2019, jijini Dar es Salaam, ukilenga kuongeza uwekezaji katika sekta ya mifugo ili kufikia mafanikio ya kweli.

Akifafanua kuhusu mpango huo, ofisa mifugo mkuu, Nathaniel Mbwambo, amesema Serikali inapaswa kuongeza uzalishaji wa nyama kutoka tani 394,600 za 2016/17 hadi tani 742,500 ifikapo mwaka 2021/22.

“Katika tasnia ya maziwa, iongeze idadi ya ng'ombe wa maziwa kutoka 782,992 mwaka 2016/17 hadi 2.98 milioni mwaka 2021/22, ili kuongeza uzalishaji wa maziwa kutoka lita bilioni mbili za sasa hadi lita bilioni 3.8,” alisema Mbwambo.

Amesema kati ya viwanda vya ngozi tisa, viwanda sita ndiyo vinafanya kazi hivyo kuna haja ya kuongeza viwanda zaidi.

Katika kuchangia mpango huo, Mbwambo alisema Serikali itachangia Sh502.6 bilioni sawa na asilimia 36 huku sekta binafsi ikichangia Sh891.3 sawa na asilimia 64.

Mratibu wa dawati la sekta binafsi katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Stephen Michael amesema mpango huo ambao ni sehemu ya Program ya Kuendeleza Kilimo (ASDP 2) umegawanywa katika kanda tatu ambazo Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na Kanda ya Kati.



Chanzo: mwananchi.co.tz