Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpango azindua kampeni mpya NMB

Dkt Phillip Mpango Xmass.jpeg Mpango azindua kampeni mpya NMB

Mon, 27 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Philip Mpango ameziagiza Halmashauri kwa kushirikiana na TFS kuzingatia kupanda aina za miti ambazo zinaendana na mazingira ya maeneo waliyopo pamoja na kuiwezesha jamii hususani ya Vijana kupata elimu zaidi kuhusu utunzaji wa miti ili kuchangia uhifadhi wa mazingira kwa weledi.

Makamu wa Rais ameyasema haya akiwa eneo la Mtumba, Dodoma leo March 27 akizundua Kampeni ya kupanda miti kitaifa kwa hisani ya Benki ya NMB ikishirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na kusisitiza kuwa Wakurugenzi wa Halmashauri zote Nchini wanapaswa kutoa maelekezo kwa Shule, Taasisi mbalimbali na kwa Wananchi ili washiriki kikamilifu katika uhifadhi na usafi wa mazingira.

Dr. Mpango ambaye amesifu jitihada za NMB ameitaka pia Benki hiyo kuona uwezekano wa kutumia umoja wa Mabenki (TBA) kuongeza nguvu zaidi katika kuifanya Dodoma ambayo ndio Makao Makuu ya Nchi kuwa ya kijani kwa muda mfupi zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live