Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpango ataka mabadiliko ya sheria ukuaji uchumi

Dkt Phillip Mpango Xmass.jpeg Mpango ataka mabadiliko ya sheria ukuaji uchumi

Mon, 6 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MAKAMU wa Rais Dk. Philip Mpango ametoa wito kwa Nchi Zinazoendelea za Kipato cha Chini (LDCs) kuhakikisha zinafanya maboresho ya kina ya kisera, kisheria na kitaasisi ili kuchochea ukuaji wa uchumi, kukuza sekta binafsi, kuongeza uwekezaji pamoja na kuleta mageuzi ya kiteknolojia.

Makamu wa Rais amesema hayo leo tarehe 05 Machi 2023 wakati akihutubia Mkutano wa Tano wa Umoja wa Mataifa wa Nchi Zinazoendelea za Kipato cha Chini unaofanyika Doha Nchini Qatar. Ameongeza kwamba ili kufikia na kutimiza Maazimio ya Doha ni muhimu mataifa yanayoendelea ya kipato cha chini kuwekeza zaidi katika rasilimali watu ya vijana na wanawake pamoja kuhakikisha zinaweka mkazo katika elimu bora, ujuzi, huduma za afya na miundombinu ikiwemo nishati, reli, bandari na tehama.

Pia Dk. Mpango amesisitiza kuimarisha ushirikiano baina ya nchi na nchi, kikanda na kimataifa pamoja na kuhakikisha nchi hizo zanapata fedha za kutosha za masharti nafuu kutoka katika Taasisi za Fedha za kimataifa na washirika wa maendeleo.

Makamu wa Rais ameeleza changamoto mpya zilizoikumba dunia ikiwamo janga la UVIKO, athari za mabadiliko ya tabia nchi na migogoro ya kimataifa ambazo zimezifanya nchi za kipato cha chini kupiga hatua hafifu katika utekelezaji wa maazimio ya Mkutano kama huo uliofanyika jijini Instambul Uturuki miaka kumi iliyopita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live