Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpango amwakilisha Samia Jukwaa la Uchumi Duniani

7e7630608b5cb030eb42e77705cf6f6a Mpango akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Dk.Abdallah Possi

Mon, 23 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango amewasili nchini Uswisi kumwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani lililotarajiwa kuanza jana Davos nchini humo.

Dk Mpango aliwasili jijini Zurich juzi na na katika mkutano huo atahudhuria mikutano inayohusu masuala ya biashara na uwekezaji, ulinzi na usalama, usalama wa chakula, mazingira na mabadiliko ya tabianchi.

Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani unahudhuriwa na wakuu wa nchi na serikali, wawakilishi wa mashirika ya kimataifa, wakuu wa taasisi, kampuni na wafanyabiashara.

Viongozi hao watajadili masuala kadhaa zikiwamo mbinu za kukabili athari za janga la Covid-19 zikiwamo za kiuchumi, mikakati ya kukabili athari za mabadiliko ya tabianchi na namna dunia inavyoweza kushirikiana katika masuala ya teknolojia na ubunifu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live