Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpango aguswa, ni kuhusu korosho ghafi

Mwenyeji Korosho Mpango aguswa, ni kuhusu korosho ghafi

Wed, 11 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Philip Mpango amezindua Kongamano la Kimataifa la Korosho huku akitaka juhudi zaid kufanyika ili kuongeza thamani katika uzalishaji wa zao hilo.

Dk Mpango amesema inashangaza kuona asilimia 90 ya korosho ikisafirishwa katika masoko ya nje bila kuongezewa thamani.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati akizindua kongamano hilo leo Jumatano Oktoba 11, 2023 jijini Dar es Salaam, kongamano ambalo litajikita kujadili fursa na ufumbuzi wa changamoto katika uzalishaji wa korosho.

“Matokeo ya kusafirisha korosho ghafi ni kupoteza ajira ambazo zingepatikana kwenye mnyororo wa thamani kwa bidhaa zitokanazo na korosho kama juisi, mvinyo, “amesema akifafanua:

“Lakini nimefurahishwa na hatua zinazoendelea kwa ajili ya kuimarisha uwekezaji wa viwanda vya kubangua korosho.”

Dk Mpango ameshauri mataifa ya Afrika kutumia masoko ya ndani ya korosho na kuondoa vikwazo ili kukuza mchango wa sekta hiyo katika uchumi.

Kongamano hilo la siku mbili, linafanyika kwa mara ya kwanza kimataifa likikutanisha makundi ya wakulima, viongozi wa mikoa mitano husika katika uzalishaji wa korosho.

Pia kuna watunga sera, sekta ya fedha, watafiti, mabalozi, wabunge, taasisi za Serikali na uwakilishi wa mataifa ya Bukinafaso, Ghana, India, Kenya, Uganda, Msumbiji, Zimbabwe, Nigeria, Afrika Kusini, Uholanzi, Hispania na Benini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live