Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpango: Ushirikiano kuimarisha kilimo endelevu

Mpangoooo WA0013 Mpango: Ushirikiano kuimarisha kilimo endelevu

Thu, 18 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe. Dk Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Kampuni ya Kimataifa ya YARA wakiongozwa na Rais, ambaye pia Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo , Svein Tore Holsether, mazungumzo yaliyofanyika kando ya Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) unaofanyika Davos nchini Uswisi.

Katika Mazungumzo hayo, Makamu wa Rais ameihakikishia kampuni hiyo kwamba serikali itaendelea kuiunga mkono katika kufanya shughuli zake nchini Tanzania.

Amesema dhamira ya serikali ni kuendelea kujizatiti kuwa ghala la chakula kikanda kwa kuzingatia ongezeko la watu pamoja na mahitaji ya chakula.

Makamu wa Rais ametoa wito wa kuongeza ushirikiano zaidi baina ya kampuni hiyo na Tanzania katika maeneo mbalimbali, ikiwemo uwekezaji katika miundombinu ya kilimo kama vile maghala, usafirishaji pamoja na umwagiliaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live