Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpango: Matunda Handeni kutafutiwa soko

Philip Mpango Makamu Mpango: Matunda Handeni kutafutiwa soko

Wed, 21 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango ameiagiza wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na uongozi wa mkoa wa Tanga kuchukua hatua za mapema katika kukabiliana na changamoto ya soko la matunda yanayozalishwa mkoani humo.

Dkt. Mpango ametoa agizo hilo mkoani Tanga alipokuwa akizungumza na Wananchi wa Kabuku wilayani Handeni akiwa kwenye ziara mkoani humo.

Ametaka kufanyika kwa tathmini ili kutambua kiasi cha matunda yanayozalishwa katika eneo hilo.

Aidha Makamu wa Rais amemuagiza Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara kukutana na wamiliki wakubwa wa viwanda vya kuchakata matunda ili waweze kutumia matunda yanayozalishwa wilayani ya Handeni na mkoa wa Tanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live