Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mongela ataka miundombinu imara ya masoko Arusha

E6107592b2785f8c59a96580f2a73732 Mongela ataka miundombinu imara ya masoko Arusha

Sat, 17 Jul 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MKUU wa Mkoa wa Arusha, John Mongela amesema ujenzi wa miundombinu bora ya biashara katika maeneo ya masoko ni jambo la muhimu na kwamba ni lazima ijengwe imara yenye uwezo wa kuishi zaidi ya miaka 50 ijayo.

Amesema masoko mengi katika jiji la Arusha yamepitwa na wakati na suluhisho pekee ni kujenga masoko ya kisasa yatakayowezesha wafanyabiashara kufanya biashara kwa nafasi na kulipa kodi zao ili kuongeza kipato na kuchangia kukuza uchumi wa nchi.

Alisema hayo baada ya kusikiliza kero za wananchi katika tarafa ya Themi, kata ya Levolosi, eneo la Kilombero juzi.

“Malengo ya ujenzi wa miundombinu bora yatafikiwa kwa ushirikiano baina ya viongozi na wananchi. Rais Samia Suluhu Hassan anapenda umoja na viongozi wa mkoa wa Arusha tuna umoja hivyo tutafikia matarajio,” alisema.

Kuhusu suala la Wamachinga, Mongela alisema serikali inatambua umuhimu wa wafanyabiashara hao na kwamba watajadili na wadau mbalimbali ili kufikia suluhu ya changamoto zao, kwani mazingira bora ya biashara ni muhimu kwa maendeleo ya sekta hiyo.

Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa mkoa alivitaka vyombo vya ulinzi na usalama mkoani humo kuhakikisha ulinzi na usalama kwa wananchi wote ili wananchi waweze kuishi kwa amani na kufanya shughuli za ujenzi wa taifa.

Chanzo: www.habarileo.co.tz