Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mo Dewji atwaa tuzo ya AABLA ya Mwanaviwanda Bora wa Mwaka 2023

MO ED 0 Mo Dewji atwaa tuzo ya AABLA ya Mwanaviwanda Bora wa Mwaka 2023

Tue, 27 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mfanyabiashara na maarufu wa Kitanzania, Bilionea Mohammed Dewji 'Mo', ametunukiwa tuzo ya Mwanaviwanda Bora wa Mwaka 2023 katika Tuzo za Wafanyabiashara Wote wa Afrika (AABLA).

Mo alipokea tuzo hiyo wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo hizo kubwa zaidi za kibiashara barani Afrika, iliyofanyika Sun City, Afrika Kusini jana Juni 23.

Katika ukurasa wake wa Twitter, Mo alimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira mazuri ya biashara Tanzania, ambayo yanawezesha maendeleo makubwa ya viwanda nchini kote.

"Ninatoa shukrani zangu kwa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira chanya kwa ustawi wa biashara Tanzania," Mo alipongeza.

Hafla ya utoaji wa tuzo za AABLA 2023 iliandaliwa kwa ushirikiano na CNBC Africa. Ni tuzo zinazoendelea kuwa tuzo kubwa zaidi za kibiashara barani Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live