Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mo Dewji amshukuru JPM

69961 Pic+mo+dewj

Mon, 5 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

MWENYEKITI wa Bodi ya wakurugenzi ya Simba, Mohamed Dewji "Mo Dewji' amemshukuru Rais wa Jamhuri, John Pombe Magufuli.

Mo Dewji amemshukuru Rais Magufuli kuipa kipaumbele michezo yote nchini jambo ambalo linachangia timu kufanya vizuri.

Amesema hayo alipokuwa akisoma hotuba mbele ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini, Harrison Mwakyembe wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi uwanja wao uliopo Bunju.

Uwanja huo unatarajiwa kukamilika Oktoba mwaka huu.

"Namshukuru sana Rais Magufuli kuwekeza nguvu zake kwenye michezo na tunaahidi kutomwangusha. Nguvu yake inatupa moyo wa kupambana ili mchezo huu ukue na tufike mbali zaidi hata kimataifa, hivyo hatutamwangusha," amesema Mo Dewji, ambaye ndiye mwekezaji wa Simba akimiliki asimilia 49 kwa thamani ya Sh 20 bilioni.

Chanzo: mwananchi.co.tz