Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mnyauko wa korosho bado tishio

59517 Pic+mnyauko

Fri, 24 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mtwara. Imeelezwa kwamba watafiti wa masuala ya udhibiti wa wadudu waharibifu na magonjwa kwenye mikorosho bado  wanaendelea na utafiti ili kukabiliana na ugonjwa wa mnyauko katika mikorosho.

Akizungumza jana Alhamisi Mei 23, 2019  katika ziara ya waandishi wa habari na watafiti iliyolenga kuwajengea uwezo waandishi  kuandika habari za sayansi, teknolojia na ubunifu yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia, mdhibiti wa wadudu na magonjwa kutoka taasisi ya utafiti na Kilimo Naliendele, Dadili Majune amesema ugonjwa huo uligundulika mwaka 2012 na mpaka sasa tiba haijapatikana.

Amesema ugonjwa huo unashambulia miti ya mikorosho na kusababisha ikauke na ikionekana dalili suluhisho ni kuukata mti husika na kuuteketeza kwa moto ili usiendelee kusambaa katika miti mingine.

Huku akieleza kuwa kuna dawa zaidi ya 10 zinazoendelea kufanyiwa utafiti amesema, “Bado hatujapata tiba lakini tumefikia pazuri. Ili  ugonjwa usiendelee kusambaa ni lazima miti yenye dalili ichomwe na zana zinazotumika ni lazima zisafishwe na ikiwezeka zipitishwe kwenye moto ili kuzuia kuusambaza ugonjwa.”

Mkulima wa zao la korosho kutoka Nanyumbu, Elisha Millanzi amesema ugonjwa huo ulionekana katika maeneo yake mwaka jana na kusaidiwa na wataalamu wa kilimo.

Chanzo: mwananchi.co.tz