Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mlemavu wa macho anayeshona nguo, ataja viongozi wa nchi aliowahi kuwashonea

2699 Kushona 660x400

Wed, 7 Feb 2018 Chanzo: millardayo.com

Siku za hivi karibuni Ayo TV na millardayo.com imepata fursa ya kufanya mahojiano na Abdaa Nyangalio ambaye ni fundi wa kushona nguo ambaye ana ulemavu wa macho (kipofu) na ni mwalimu wa wanafunzi wa ushonaji ambao pia ni vipofu.

Ameeleza kuwa alipata upofu baada ya kuugua pressure ya macho yaani Trachoma mnamo mwaka 1989 na alipokuwa akitibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili daktari aliyekuwa akimhudumia ambaye alikuwa ni raia wa Urusi alimwambia anataka kumfundisha kushona akiwa hivyo hivyo kipofu.

“Nilikubali kujifunza na ndani ya miezi mitatu nilikuwa nimeshaweza kabisa kushona, nimeshonea viongozi mbalimbali suti ikiwa ni pamoja na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na viongozi wengine wengi na watu maarufu.” – Abdallah Nyangalio



MAKJUICE: KAANZA NA MTAJI WA ELFU 7 MPAKA DALADALA YA KUUZA JUICE MTAANI



Rafiki wa Kingunge “Dakika 15 baada ya kuzikwa wanataka vyake wagawane”



Chanzo: millardayo.com