Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma akomalia msimamo wake dhidi ya soko la Sabasaba

W1200 H63 Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma

Wed, 20 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Licha ya wafanyabiashara wa Soko la Sabasaba Jijini hapa kutishia kuandamana hadi kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Ili kumfikishia kilio chao cha kuondolewa katika eneo hilo, Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Joseph Mafuru ameendelea kuwataka wafanyanishara hao kupisha ukarabati wa soko hilo huku akieleza lengo la serikali ni jema kwa maslahi ya wafanyabaishara hao na siyo vinginevyo.

Hayo yanajiri ikiwa ni hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka kuagiza Jiji la Dodoma kufanya mkakati wa Uboreshaji wa Soko hilo kwa kuwaorodhesha wafanyabiasha wote katika mfumo maalum ili kuweza kuondoa migogoro inayoweza kujitokeza hapo baadaye.

Akiongea na waandishi wa habari leo Aprili 20, 2022 Ofisini kwake amesema lengo la Jiji ni kuwahamisha kwa muda wafanyabiashara hao ili kufanya ukarabati wa soko hilo na baada ya ujenzi huo kukamilika watawarudisha kuendelea na shughuli zao kama kawaida.

"Zoezi hili tunalifanya kwa uwazi,tuliwashirikisha wafanyabiashara wote na kilichobaki sasa ni kuhakiki ili kuwatambua nani anamiliki nini na anafanya nini na kuwaondoa hofu kuwa tunakwenda kuwahamisha kwa muda ili kupisha ujenzi wa eneo hilo kwa muda wa mwaka mmoja au miwili kulingana na mchoro wetu”amesema Mafuru

Aidha amesema soko hilo ni la historia na limechakaa kutokana na kuwa ni la muda mrefu tangu mwaka 1996 halijafanyiwa ukarabati wa miundominu yake hivyo ni wakati muafaka wa kuhakikisha linakarabatiwa kisasa zaidi kulingana na mahitaji na kuweza kuhudumia zaidi ya wafanyabiashara 7000 .

"Lengo la jiji ni kuboresha mazingira ya wafanyabiashara na si kuwadhulumu,imefika wakati wafanyabiashara kuelewa Dodoma Sasa ni Jiji na ndiyo Makao makuu ya nchi na soko la Sabasaba limekuwa halina hadhi lazima tufanye ukarabati,"amefafanua na kuongeza;

Chanzo: www.tanzaniaweb.live