Arusha. Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Azam Media Ltd, Abdul Mohammed leo Jumamosi Mei 18, 2019 amechaguliwa kuwa mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa Benki ya CRDB.
Abdul ambaye pia ni ofisa mtendaji mkuu wa timu ya mpira wa miguu ya Azam FC amechaguliwa baada ya kupata asilimia 16.86 ya kura za wanahisa wa benki ya CRDB.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo mwenyekiti wa kikao cha wanahisa jijini Arusha Jaji mkuu mstaafu, Augustine Ramadhani amesema wengine waliochaguliwa ni Ally Hussein Laay.
Laay, aliyekuwa mwenyekiti bodi iliyopita alipata asilimia 27.52 ya kula. Wengine waliochaguliwa ni Martin Warioba aliyepata asilimia 50.62 ya kura na Boniface Mahegi aliyepata asilimia 27.42.
Wagombea 16 walishiriki uchaguzi huo katika makundi tofauti kulingana na viwango vya hisa.
Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amewapongeza wajumbe hao kwa kuchaguliwa na kuahidi kuwapa ushirikiano kufanikisha benki hiyo kuendelea kuongoza nchini.
Pia Soma
- Rais Kenyatta aja na mkakati mpya wa uchumi wa kidigitali
- Dk Kigwangalla agoma kulipunguza pori la akiba la Maswa
- LHRC yatua Kigoma kutoa elimu ukatili wa kingono