Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkumbo: Uchumi umekuwa kwa asilimia 6

Mkumbo Biz Mkumbo: Uchumi umekuwa kwa asilimia 6

Thu, 9 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Profesa Kitala Mkumbo amesema katika miaka mitatu iliyopita uchumi wa Tanzania umekua ukiimarika na ukuaji kwa sasa umefikia asilimia sita.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha kuunganisha malori na matipa cha Satarn kilichopo Kigamboni mkoani Dar es Salaam, Profesa Mkumbo amesema uchumi wa Tanzania unaimarika kutokana na uwekezaji uliofanywa na Serikali katika kilimo na ujenzi wa Miundombinu.

Profesa Mkumbo amesema sekta ya viwanda imekuwa na mchango chini ya asilimia 10 katika miongo mitatu iliyopita lakini kwa sasa changamoto nyingi zimetatuliwa na ndio maana uwekezaji katika sekta hiyo unazidi kukua.

Amesema kuwa katika miradi 526 iliyosajiliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania kwa mwaka jana pekee, miradi 237 ilikuwa ni ya uzalishaji viwandani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live