Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkulima wa vitunguu Iringa aiangukia Serikali

59340 Vitunguupic

Fri, 24 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Serikali imeombwa kuingilia kati changamoto inayoyumbisha soko la wakulima wa vitunguu maji Mkoani Iringa.

Imeelezwa kuwa hali hiyo inawakatisha tamaa wakulima wengi vijana walioingia kwenye fursa ya kilimo hicho.

Haidari Kuchimba, ameyasema hayo usiku huu wa Alhamisi Mei 23, 2019 katika mjadala wa Jukwaa la Fikra linaloandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL).

Mkulima huyo anayetokea Kijiji cha Msosa kilichopo Ruaha Mbuyuni mkoani Iringa, amesema hali iliyopo kwa sasa inakatisha tamaa.

“Tunahitaji Serikali itusaidie kufahamu hasa wateja wanataka aina gani ya vitunguu maji, kwa sababu unaweza kulima vitunguu vyekundu ukakuta soko linataka vitunguu vya rangi ya  papo, kibaya zaidi, hata bei haieleweki.

“Wakulima tunaumia Sana Iringa, gharama tunazotumia kwenye uzalishaji wa vitunguu zinakuwa kubwa tofauti na matarajio ya bei sokoni, kwa hiyo faida inakuwa ndogo Sana,” amesema Kuchimba.

Habari zinazohusiana na hii

Kuchimba amesema endapo Serikali itaingilia kati, itasaidia kukuza uzalishaji, kupanua soko na ajira.

Amesema changamoto nyingine ni kukosekana kwa viwango halisi vya bei ya pembejeo zinazowafikia kwa ajili ya msimu wa uzalishaji.

Kwa mara ya kwanza jukwaa hili lilifanyika Juni 28, Mwaka jana likiwa na mada ya Afya Yetu, Mtaji wetu.

Awamu ya pili lilifanyika Oktoba 4, mwaka jana likiwa na mada inayohusu fursa na changamoto kuelekea uchumi wa viwanda.

Na awamu ya tatu lilifanyika Februari 7, mwaka huu likiwa na mada inayohusu Mkaa, Uchumi na Mazingira yetu.

 

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz