Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkonge kuuzwa soko la utalii Zanzibar

Images (18) Mkongee.jpeg Mkonge kuuzwa soko la utalii Zanzibar

Thu, 12 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika mwendelezo wa kuhamasisha matumizi ya bidhaa za mkonge nchini, Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), imedhamiria kulifanya zao hilo kuwa zao la kitalii ambapo inatarajia kuingiza bidhaa zinazotokana na zao hilo katika Soko la kitalii kupitia vijana kutoka visiwani Zanzibar.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa TSB, Saddy Kambona alipokuwa akizungumza wakati wa kuhitimisha mafunzo maalumu kwa vijana kutoka katika Chuo cha mafunzo Zanzibar na Wanachama wa klabu ya mkonge ya shule ya sekondari Coastal Tanga kuhusu sekta ya mkonge.

Aidha, wamehitimisha mafunzo ya ndani ya kujadiliana juu ya fursa mbalimbali zinazotokana na mkonge ambazo Wazanzibar wanaweza wakazitumia ambapo lengo ni kuhakikisha wanamsaidia Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika kuondoa changamoto ya ajira hususani kwa vijana na kina mama.

“Kwa kuwa Zanzibar ni ardhi ya karafuu si rahisi kulima mkonge hivyo tunaweza tukatumia mkonge kutoka Tanzania Bara kwa kutumia soko la utalii la Zanzibar kuzalisha bidhaa mbalimbali.

Pamoja na mambo mengine, amesema kwa sasa bodi imeona inaweza kuwapelekea bidhaa za mkonge huko huko Zanzibar ili watumie zao hilo badala ya makumbi ya nazi ambayo wanayatumia sasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live